SHAIRI LA; MAISHA YANGU
Matangazo mnanitangazia, utamu kunivutia
Starehe naipenda, maisha yanasonga.
Tatizo naambiwa, starehe ina madhara
Kivipi nikuamini, wakati wakataza nawe waipenda?
Kinywaji ni kitamu, tena ladha yake mithili ya dhahabu
Nani nimwamini, zaidi ni kunywa kulewa na kupumzika.
Nyumbani watoto wangu, chakula ni ugali maharagwe
Mie zangu ni nyama, tena nundu na meza kujaa kilevi
Kama nina mke wangu, naweza kukaa naye mchana
Ila sasa hivi ni usiku, naelewa huyu nayekunywa naye atanifaa.
Kwa viburudisho vya kutosha, tena vya kupendeza nafsi
Kwa maisha ya kila siku, nalewa tena kuridhika.
Kweli kupenda napenda, ila ni matatizo ya dunia
Nani kilio chetu kukisikia, kama nisipolisemea kila wakati.
Usinifurahie kwa kuwa nacheka, ni mengi nayasitiri moyoni
Kwamwe sungura hashikiki, bali kwa kutumia akili na mipango.
Adui yetu mkubwa ni ujinga, na si umasikini akilini mwetu
Tukimshinda adui yetu ujinga, tutaweza kumpiga maradhi.
Tukimshinda adui yetu ujinga, tutaweza kumpiga umasikini
Tukimshinda adui yetu ujinga, tutaweza kumpiga rushwa.
Mdomo wangu muda wote umejaa, kazi kwangu kutafuna
Kwani kazi ni nyingi na maisha magumu, we acha kwani?
Nahitaju kupumzika tatizo, pesa ya kesho nitapata wapi?
Nahitaji kuoa ila pesa wapi, ngoja nitafune usingizi niukose.
Maisha yakiwa magumu, kulala nahisi suluhisho
Nikitumia nahisi itasaidia, madhara siyaoni usingizi mwema.
Nakuhitaji uje karibu, ila kwa kawaida siwezi kujiajiri
Ubunifu wako utanipa ajira, ila kukuibia ndio kauli yangu.